1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Mpango wa amani Gaza utaendelea kutekelezwa

22 Oktoba 2025

Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance amesema ana matumaini makubwa kuwa makubaliano ya amani huko Gaza yataendelea kutekelezwa.

Israel  | Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance akiwa ziarani huko Israel
Makamu wa Rais wa Marekani JD Vance akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa ziarani nchini IsraelPicha: Nathan Howard/REUTERS

Vance ameitoa kauli hiyo wakati akiendelea na ziara yake huko Israel yenye lengo la kupata uungwaji mkono kwa mpango huo pamoja na ujenzi mpya wa eneo hilo la Wapalestina lililoharibiwa na vita.

Licha ya wasiwasi wa Israel kwamba Hamas itatumia muda huu wa usitishwaji mapigano ili kujiimarisha tena huko Gaza,  JD Vance amesema chini ya makubaliano hayo, Marekani haitaweka muda wa mwisho kwa kundi hilo kukamilisha zoezi la kupokonywa silaha.

Hayo yanajiri baada ya Rais wa Marekani  Donald Trump  kuonya kuwa mataifa washirika katika eneo hilo la Mashariki ya Kati yataivamia Gaza ili kuiangamiza Hamas iwapo itashindwa kutekeleza kikamilifu makubaliano hayo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW