Marekani inamatumaini kuhusu azimio la UN Gaza
13 Novemba 2025
Matangazo
Azimio hilo linaunga mkono hatua ya kupelekwa kwa kikosi cha kimataifa cha kulinda amani.
Rubio amesisitiza kuwa hatua muhimu zinapigwa na muafaka utapatikana hivi karibuni.
Huku hayo yakijiri, Rais wa Israel Isaac Herzog, pamoja na maafisa waandamizi wa jeshi, wamelaani vitendo vya walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu, wakitaka kukomeshwa mara moja vitendo hivyo vinavyoongezeka.
Herzog aliyaelezea mashambulizi hayo kama "ya kushangaza na "makubwa". Naye Marco Rubio amesema vurugu hizo zinaweza kuathiri mpango wa amani wa Gaza.