Marekani inasema huenda ikazungumza na Korea ya kaskazini,Pyongyang ikikubali kurejea katika meza ya mazungumzo ya pande sita
8 Julai 2006Marekani inaunga mkono pendekezo la jamhuri ya umma wa China la kuitishwa mazungumzo ya pande sita kuhusu Korea ya kaskazini.Mjumbe wa Marekani Christopher Hill amesema mjini Seoul-Korea ya kusini,ikiwa Korea ya kaskazini itaacha kuyasusia mazungumzo hayo,inawezekana pakaafunguka njia pembezoni mwa mazungumzo hayo kufanyika mkutano wa pande mbili kati ya wawakilishi wa Marekani na Korea ya kaskazini.Serikali ya Pyongyang inapinga tangu miezi sita sasa kushiriki katika mazungumzo ya pande sita pamoja na Korea ya kusini,Marekani,jamhuri ya umma wa China,Japan na Urusi.Jumatano iliyopita Korea ya kaskazini imefanya majaribio zaidi ya sita ya maakombora ya kinuklea.Japan imewasilisha mswaada wa azimio mbele ya baraza la usalama ikidai Korea ya kaskazini iwekewe vikwazo vya kiuchumi.