MAREKANI IONDOSHE USHURU WA CHUMA PUA:
21 Novemba 2003Matangazo
BEIJING: Uchina imemuita balozi wa Marekani mjini Beijing kulalamika dhidi ya mpango wa serikali ya Bush wa kutaka kuweka vikomo kwa biashara ya nguo na vitambaa kutoka Uchina.Kwa kuchukua hatua hiyo Marekani inataka kuhifadhi nafasi za kazi katika viwanda vya nguo nchini Marekani.Naibu waziri wa kigeni wa Uchina Zhou Wenzhong amesema Uchina "imeshtushwa na hatua hiyo ya Marekani".Vile vile ameitaka Washington ifuate amri mpya ya Shirika la Biashara Duniani WTO na iondoshe ushuru unaotozwa na Marekani kwa chuma cha pua kinachoagiziwa kutoka nchi za ngámbo.Umoja wa Ulaya pia umeitaka Marekani iondoshe ushuru huo.
