MAREKANI ISIINGILIE MAMBO YA NDANI:
11 Januari 2004Matangazo
BEIJING: Uchina imetoa muito kwa Marekani kuwa iache kuingilia mambo ya ndani ya mamlaka yake.Hayo ni kwa mujibu wa shirika rasmi la habari nchini Uchina.Muito huo umetolewa baada ya wizara ya kigeni ya Marekani kuhimiza kuwa Hong Kong iwe na udemokrasia zaidi.Msemaji wa wizara ya kigeni ya Uchina amesema masuala ya Hong Kong na mambo ya ndani ya Uchina,na serikali ya Beijing inapinga kabisa serikali yo yote ile ya kigeni kuingilia kati.Hong Kong-koloni la zamani la Uingereza ilirejea chini ya utawala wa Uchina katika mwaka 1997.Sasa Hong Kong ni eneo maalum lenye uongozi wake wenyewe chini ya serikali ya Uchina.
