Marekani: Israel imruhusu Mkuu wa UNRWA kutembelea Gaza
20 Machi 2024Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Vedant Patel amesema, imani yao ni UNRWA iweze kufanikiwa kutembelea eneo la oparesheni, na kwamba wataendelea kushirikiana na serikali ya Israel ili kuidhinisha vibali vya wafanyazi wa Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada.
Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini alisema siku ya Jumatatu mjini Cairo kuwa, ana nia ya kutembelea katika mji wa Kusini mwa Gaza Rafah, lakini ombi lake halikukubaliwa na Israel.
Soma pia:UN yaonya juu ya vitendo vya Israel kuzuia misaada kuingizwa Gaza
Israel imedai wafanyakazi wa shirika hilo walihusika na shambulio la Oktoba 7, na kuchochea kampeni kubwa ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza.
Marekani imesitisha ufadhili kwa UNRWA na kupisha uchunguzi, lakini imesema kazi ya shirika hilo ni ya thamani.
Sikiliza habari nyingine zaidi za ulimwengu kwenye chaneli yetu ya YouTube hapa.