SiasaAsia
Makombora ya Korea kaskazini yanakiuka maazimio ya UN
15 Julai 2023Matangazo
Katika taarifa ya pamoja, wanadiplomasia wakuu wa Marekani, Korea Kusini na Japan wameeleza kuwa urushaji wa kombora hilo kunatishia amani sio tu katika rasi ya Korea bali katika sehemu nyingine za dunia.
Nchi hizo tatu zimeihimiza Korea Kaskazini kukomesha kile walichokiita "uvunjaji wa sheria na kuchochea mzozo wa kidiplomasia, na badala yake inafaa kurudi kwenye mazungumzo."
Soma zaidi: Korea Kaskazini yafanya jaribio la kombora la masafa marefu
Kombora hilo, lililorushwa kwenye pwani ya mashariki ya Korea Kaskazini, liliruka kwa muda wa dakika 7 na kwa umbali wa kilomita 1,000 katika kile kinachoelezwa kuwa muda mrefu zaidi wa kombora la Korea Kaskazini kukaa angani.