1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Marekani, Japan na Korea zaweka makubaliano mapya ya usalama

18 Agosti 2023

Marekani, Japan na Korea Kusini zimekubaliana kutia saini makubaliano mapya ya usalama yatakayozipelekea nchi hizo tatu kushauriana panapokuwa na mzozo wa kiusalama au kitisho katika ukanda wa Pasifiki.

Makubaliano hayo yanalenga kudhibiti kitisho chochote cha usalama katika kanda ya Pasifiki.
Makubaliano hayo yanalenga kudhibiti kitisho chochote cha usalama katika kanda ya Pasifiki.Picha: South Korean Defense Ministry/UPI Photo/IMAGO

Hayo yamesemwa na maafisa katika serikali ya Rais Joe Biden.

Taarifa hizo zimejitokeza wakati ambapo Rais Biden anajiandaa kukutana na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol na Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida, katika mkutano wa kilele huko Camp David, Maryland.

Makubaliano hayo ni mojawapo ya juhudi kadhaa za pamoja ambazo viongozi hao wanatarajiwa kuiztangaza katika mkutano huo wa kilele wa siku nzima.

Mataifa hayo matatu yanapania kuongeza ulinzi na mahusiano ya kiuchumi wakati ambapo kuna ongezeko la kitisho cha mashambulizi ya nyuklia kutoka kwa Koea Kaskazini na uchokozi wa China katika eneo la Pasifiki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW