Marekani: Jiji la Texas lakabiliana na wimbi la wahamiaji
30 Aprili 2023Maelfu ya wahamiaji kutoka Mexico, wanawapa kazi ngumu maafisa wa Marekani kuhudumia makundi makubwa ya watu wanaokimbia umaskini na vurugu kwenye nchi yao.
Wahamiaji wengi waliofika katika mji wa Brownsville kusini mwa Texas wamepelekea watoa huduma za kijamii kuelemewa na kusababisha kukataliwa baadhi ya wahamiaji katika sehemu za kuwasaidia watu hao. Maafisa wamesema zaidi ya wahamiaji 15,000, wengi wao kutoka Venezuela, wiki iliyopita walivuka mto ulio karibu na mji huo wa Brownsville kinyume cha sheria.
Soma pia: Biden aongeza idadi ya wakimbizi wanaoingia Marekani
Maafisa wa Forodha na Ulinzi wa Mipaka katika jimbo la Texas wamesema hilo ni ongezeko kubwa la wahamiaji ukilinganisha na watu 1,700 walioingia kwenye eneo hilo wiki mbili za kwanza za mwezi huu wa Aprili.