1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuisaidia Georgia

10 Mei 2005

Tbilis:

Rais George W. Bush wa Marekani amesema leo mjini Tbilis kuwa mapinduzi ya amani ya Georgia ya mwaka 2003 ni mfano mzuri wa kuigwa na nchi nyingine zinazopigania demokrasia. Urussi itanufaika zaidi kuwa na nchi za kidemokrasia katika mipaka yake. Rais Bush akiwahutubia watu zaidi ya 150,000 katika uwanja wa uhuru mjini Tbilis amesema kuwa Marekani inaunga mkono ujenzi wa Georgia iliyo huru na ya kiliberali. Rais wa Marekani amesema kuwa mapinduzi ya waridi yana nguvu za kihistoria kwa sababu hayakuwatia moyo Wageorgia peke yao isipokuwa watu wengine pia duniani. Rais Bush ameongeza kusema kuwa wakati unapokuwa na nchi za amani katika mipaka yako ndivyo ambavyo utaweza kunufaika. Ana matumaini kuwa Urussi itatambua manufaa ya kuwa na nchi za kidemokrasia katika mipaka yake. Bush ni Rais wa kwanza wa Marekani kulitembelea eneo la Caucasus ambalo kwa muda mrefu limekuwa chini ya ushawishi wa Urussi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW