Marekani kuishambulia Iran iwapo italipiza kisasi
6 Januari 2020Iran imepeleka ujumbe wa nguvu kwa Marekani na duniani kote baada ya ibada ya wafu kwa ajili ya jenerali Soleimani iliyofanyika kwenye mji wa Ahwaz uliochaguliwa na familia yake. Mji huo wa kusini magharibi ulikuwa uwanja wa vita vya Iran na Irak mnamo miaka ya 80 na pia hapo ndipo jenerali Soleiman alipoanza kazi ya uaskari.
Mji huo pia ni maarufu kutokana na maandamano ya kuipinga serikali ya mnamo mwezi wa Novemba. Mwili wa jenerali Soleimani ulipokewa kwa muziki wa kisasa:
Mtu mmoja aliehudhuria mazishi hayo amesema si familia ya Soleimani peke yake inayoomboleza bali ni taifa lote la Iran. Watu wengi waliohudhurua mazishi walikuwa na ghadhabu juu ya mauaji yaliyofanywa na Marekani.
Mama mmoja amesema jenerali Soleiman alikuwa kama kaka yake, mama huyo ameeleza kuwa jenerali Soleimani alitoa maisha yake kwa ajili ya kuulinda mustakabal wa mtoto wa mama huyo. Watu wa Iran wamekasirishwa sana na mauaji ya jenerali huyo na wanayatoa machungu yao wazi wazi.
Mwombolezaji mwingine amemwambia Trump awe tayari kwani Marekani na Rais wake Trump wanapaswa kujua kwamba Wairan watalipiza kisasi cha uhakika na kwamba Trump sasa lazima aanze kukiogopa hata kivuli chake mwenyewe. Maalfu ya Wairan waliohudhuria mazishi walipiga mayowe kutaka Marekani iteketezwe.
Awali wabunge wa Iran walikutana kwenye mji mkuu,Tehran. Wabunge hao pia walionyesha hasira zao juu ya kuuliwa kwa jenerali Soleimani. Kutokana na mazishi shughuli muhimu zilifungwa kwenye mji wa Ahwaz. Watu wote wa mji huo walipata fursa ya kuhudhuria maombolezo. Mwili wa Jenerali Soleimani ulipelekwa mjini Tehran kwa matayarisho ya kuepelekwa kwenye mji mtakatifu wa Qom. Baada ya hapo mwili wake ulipelekwa kwenye mji wake wa uzawa wa Kerman kwa ajili ya mazishi.
Chanzo:/Senz, Karin (ARD Istanbul)