1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kuishambulia Siria

18 Februari 2005

Washington:

Serikali ya Marekani, kutokana na mvutano uliopo kati yake na Siria, haiondoi uwezekano wa kutumia nguvu dhidi ya nchi hiyo. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, Bibi Condoleezza Rice, amesema mjini Washington kuwa Rais George W. Bush anafikiria mikakati kadhaa ya kupambana na Siria. Isitoshe, serikali ya Marekani imeiomba jamii ya kimataifa ishinikize Siria ili iondoe Wanajeshi wake nchini Lebanon. Marekani inawashuku Wanajeshi wa Siria walioko Lebanon kuwa wanahusika na kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo Rafik Hariri. Isitoshe inailaumu Siria kuwa inakumbatia ugaidi wa kimataifa na ina hatarisha amani ya Mashariki ya Kati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW