1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kushambulia zaidi makundi yanayoungwa mkono na Iran

5 Februari 2024

Marekani imesema inakusudia kuanzisha mashambulizi zaidi dhidi ya makundi yanayoungwa mkono na Iran katika eneo la Mashariki ya Kati.

Marekani I Jake Sullivan akizungumza na wanahabari
Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama katika Ikulu ya White House Jake Sullivan akizungumza na waandishi wa habari Desemba 4, 2023Picha: Evan Vucci/AP/picture alliance

Hayo yameelezwa jana na mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama katika Ikulu ya White House Jake Sullivan.Sullivan amesema mashambulizi hayo yanalenga kutuma ujumbe ulio wazi kwamba Marekani itajibu vikali ikiwa itashambuliwa na wanajeshi wake kuuawa.

Tamko hilo linajiri siku mbili tu baada ya Marekani  kufanya mashambulizi dhidi ya makundi yanayofungamana na Iran  katika nchi za Iraq, Syria na Yemen.

Marekani na Uingereza zilianzisha mashambulizi dhidi ya maeneo yapatayo 36 yanayomilikiwa na waasi wa Houthi nchini Yemen. Wiki iliyopita, wanajeshi watatu wa Marekani waliuawa katika shambulio la droni kaskazini-mashariki mwa Jordan.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW