1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kutuma ujumbe usio rasmi Taiwan baada ya uchaguzi

Sylvia Mwehozi
11 Januari 2024

Marekani inakusudia kutuma ujumbe usio rasmi huko Taiwan baada ya uchaguzi muhimu katika kisiwa hicho kinachojitawala na kuionya China dhidi ya uchokozi wowote wa kijeshi.

Taiwan Wahl 2024 | Tsai Ing-wen
Rais wa Taiwan Tsai Ing-wen akiwapungia mkono wafuasi wakati wa mkutano wa kampeni za mgombea urais wa chama tawala cha Democratic Progressive Party (DPP) Lai Ching-te mjini New Taipei.Picha: Ann Wang/REUTERS

Marekani inakusudia kutuma ujumbe usio rasmi huko Taiwan baada ya uchaguzi muhimu katika kisiwa hicho kinachojitawala na kuionya China dhidi ya uchokozi wowote wa kijeshi. Hatua hiyo ya Washington inajiri huku kukiwa na mvutano unaozidi kuongezeka kuhusu uchaguzi wa Jumamosi.

Afisa mmoja mwandamizi katika utawala wa Rais Joe Biden, aliyezungumza na waandishi wa habari kwa sharti la kutotajwa jina, alisema Washington haiungi mkono upande wowote katika uchaguzi huo.

Fahamu wagombea wa Taiwan: Wagombea Urais Taiwan wachuana katika mdahalo kabla ya uchaguzi

Washington imeionya China dhidi ya kuzusha mvutano katika uchaguzi huo, ambao unatazamwa kwa karibu katika kuamua mustakabali wa uhusiano wa Taiwan na Beijing.

China imeapa kwamba haitakubali kamwe kuachana na dhamira yake ya kukitwaa kisiwa hicho siku moja. Taiwan itafanya uchaguzi wa rais na bunge siku ya Jumamosi,  katikati mwa mivutano ya siasa za kikanda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW