Marekani: Muhimu kuepusha vita kamili Mashariki ya Kati
6 Agosti 2024Iran iliapa kuwa inayo haki ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya wiki iliyopita ya kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh.
Shambulizi la Haniyeh ambalo Israel haijalizungumzia moja kwa moja, lilijiri saa chache baada ya shambulizi la Israel mjini Beirut kumuuwa Fuad Shukr, mkuu wa kijeshi wa vuguvu la Hezbollah nchini Lebanon, linaloungwa mkono na Iran.
Wizara ya afya ya Lebanon imesema mashambulizi ya anga ya Israel kusini mwa Lebanon, yamewaua watu watano. Duru za vikosi vya usalama vya Lebanon vimesema zimesema wapiganaji wanne wa Hezbollah ni miongoni mwa waliokufa.
Soma pia:Iran: Tunayo haki ya kuiadhibu Israel kufuatia mauaji ya Haniyeh
Nao wanamgambo wa Hezbollah wamesema walifanya leo mfululizo wa mashambulizi ya droni na makombora kaskazini mwa Israel. Hezbollah hata hivyo imeonya kuwa hatua yake inayosubiriwa pakubwa ya kulipiza mauaji ya kamanda wake mwandamizi wiki iliyopita bado haijafanywa.
Jeshi la Israel limesema droni kadhaa za adui ziligundulika zikiingia katika anga zake kutokea Lebanon na moja ikadunguliwa.