1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiMarekani

Marekani na China zafanya mazungumzo ya kibiashara

Saleh Mwanamilongo
15 Machi 2026

Mazungumzo ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani yameanza mjini Paris, Ufaransa, yakitarajiwa kuweka msingi wa ziara ya rais wa Marekani, Donald Trump, nchini China mwishoni mwa mwezi huu.

Ujerumani Munich 2026 | Mkutano wa pande mbili kati ya Marco Rubio na Wang Yi katika Mkutano wa Usalama wa Munich.
China si mwanachama wa klabu hiyo ya OECD yenye nchi 38, nyingi zikiwa demokrasia tajiri, na inajiona kama nchi inayoendelea.Picha: Alex Brandon/AFP

Ujumbe wa Marekani unaongozwa na Waziri wa Fedha Scott Bessent, huku China ikiwakilishwa na Naibu Waziri Mkuu He Lifeng. Pande hizo mbili zinajadili masuala ya pamoja ya biashara na uchumi.

Ziara ya Trump itakuwa ya kwanza ya rais wa Marekani nchini China tangu mwaka 2017, wakati alipoizuru nchi hiyo kwenye muhula wake wa kwanza. Na inakuja miezi michache baada ya Trump na Xi Jinping kukubaliana kusitisha kwa muda mgogoro wa kibiashara uliosababisha ushuru mkubwa kati ya mataifa hayo mawili.

Hata hivyo, mvutano wa kibiashara bado upo. Mazungumzo hayo pia yanaweza kugusia vita vya Iran na athari zake kwa bei na usambazaji wa mafuta duniani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW