Marekani na Denmark kukutana kujadiliana suala la Greenland
14 Januari 2026
Matangazo
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Vivian Motzfeldt pia atahudhuria kikao hicho.
Mkutano huo ulikuwa umekubaliwa katika ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje na kulingana na Waziri Mkuu wa Denmark Mette Frederikssen, Vance alifanya maamuzi ya dakika za mwisho kuhudhuria kikao hicho.
Frederiksen na Waziri Mkuu wa Greenland Jens-Frederik Nielsen walisisitiza jana Jumanne mbele ya waandishi wa habari huko Copenhagen kwamba Greenland haiuzwi na haiwezi kuunganishwa na Marekani.