1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Ethiopia wajadili uwajibikaji huko Tigray

15 Machi 2023

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Antony Blinken na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed wamejadili umuhimu wa uwajibikaji kwa ukatili uliofanywa na pande zote za mzozo mkoani Tigray kaskazini mwa Ethiopia.

Äthiopien | Permierminister Abiy Ahmed und Anthony Blinken
Picha: Fana Broadcasting Corporate S.C

Wakati wa mkutano wao katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, Blinken alielezea wasiwasi kuhusu hali katika mkoa mwingine, Oromiya, ambao umeshuhudia machafuko katika nyakati za karibuni.

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani ametangaza kuwa Marekani itaipa Ethiopia dola milioni 331 ikiwa ni katika msaada mpyawa kibinaadamu.

Soma pia:Ethiopia yatoa onyo juu ya uchunguzi wa vita vya Kaskazini

Amesema ufadhili huo utatoa usaidizi kwa watu waliopoteza makaazi na kuathirika na mapigano, ukame na uhaba wa chakulanchini Ethiopia.

Blinken ataelekea katika taifa la Afrika Magharibi la Niger hapo kesho, ambalo limekuwa likipambana na ongezeko la uasi wa itikadi kali.