Marekani na Karibiki zahimiza suluhisho la amani Haiti
14 Februari 2004Matangazo
WASHINGTON: Marekani, Kanada na Jumuiya ya Nchi za Karibiki(CARICOM) pamoja na Shirika la Nchi za Marekani (OAS) zimetoa mwito kwa Rais wa Haiti Jean Bertrand Aristide na mpinzani wake, kutafuta suluhisho la amani kwa mgogoro kisiwani humo. Katika tangazo lao la pamoja lililotangazwa mjini Washington mashirika hayo yanaiita serikali ya Haiti kuheshimu haki za raiya wote. Nao upinzani wa kisiasa unapaswa kutekeleza jukumu lake, na kuacha matumizi ya mabavu lilisema tan´gazo hilo.