Marekani na Korea kaskazini zawasiliana kuyafufua mazungumzo.
7 Juni 2005Matangazo
New York.
Marekani na Korea kaskazini zimekua na mazungumzo mjini New York yenye lengo la kuyakwamua mazungumzo yaliokwama ya mataifa sita, juu ya mpango wa silaha za kinuklea wa Korea kaskazini. Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani Sean McCormack alisema mkutano huo umetokana na taratibu za mawasiliano. Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi.Mawasiliano hayo mapya ,yamekuja mwaka mmoja baada ya kuvunjika kwa mazungumzo yalioanzishwa na Marekani, China, Korea kusini, Japan na Urusi, katika juhudi za kuishawishi Korea kaskazini isitishe mpango wake wa silaha za kinuklea.