1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Korea Kusini zapanga kusitisha Luteka za kijeshi

Zainab Aziz Mhariri: Rashid Chilumba
3 Machi 2019

Marekani na Korea Kusini zimetangaza kuwa zinasitisha luteka za kijeshi za pamoja ambazo hufanyika mara mbili kila mwaka.

Südkorea Gemeinsame Militärübung mit der USA
Picha: Getty Images/AFP/Jung Yeon-Je

Hatua hiyo ni juhudi za kufufua mazungumzo ya kidiplomasia yatakayowezesha Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa silaha za Nyuklia.

Waziri wa ulinzi wa Korea Kusini Jeong Kyeong Doo na kaimu waziri wa ulinzi wa Marekani Patrick Shanahan wamekubaliana kuwa nchi hizo mbili zitafanya mazoezi madogo ya kijeshi baadaye mwezi Machi.

Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema uamuzi huo unatoa ishara ya juhudi za pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini za kupunguza wasiwasi uliopo na badala yake kuunga mkono juhudi za kidiplomasia zitakazowezesha kuondoa silaha za nyuklia kwenye rasi ya Korea.

Rais wa Marekani Donald Trump amewahi kuzikosoa luteka hizo za kijeshi akisema kuwa ni ghali na za uchokozi kwa Korea Kaskazini. Korea Kaskazini imekuwa ikiyazingatia mazoezi hayo ya kivita kama njama ya Marekani na Korea Kusini kuivamia nchi hiyo kijeshi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW