1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani na Taiwan zasaini makubaliano ya kibiashara

2 Juni 2023

Marekani na Taiwan zimesaini makubaliano ya kibiashara licha ya upinzani kutoka China.

Symbolbild USA Taiwan
Picha: Daniel Ceng Shou-Yi/ZUMA Press/picture alliance

China inadai kisiwa hicho chenye mamlaka yake ya ndani ni sehemu ya eneo lake.

Serikali hizo mbili za Taiwan na Marekani zimesema makubaliano hayo yataimarisha mahusiano ya kibiashara kwa kuboreshwa shughuli za forodha, uwekezaji pamoja na maeneo mengine.

Makubaliano hayo yalisainiwa na wafanyakazi wa taasisi, ambazo sio rasmi katika sekta ya teknolojia ya hali ya juu, zinazoendeleza mahusiano kati  ya Marekani na Taiwan.

Taasisi hizo hazina uhusiano rasmi wa kidiplomasia ingawa zinaendeleza mahusiano yasiyo rasmi na Marekani na yanahusika kwenye biashara inayohusisha  mabilioni ya dola kila mwaka.