Marekani na UK zaendeleza mashambulizi dhidi ya wahouthi
23 Januari 2024Marekani na Uingereza wameendeleza mashambulizi yao ya pamoja ya kijeshi kwa siku ya pili leo dhidi ya waasi wa Houthi kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na waasi hao katika Bahari ya Shamu. Waasi hao wanaoungwa mkono na Iran wameapa kulipiza kisasi.
Mashambulizi ya leo yaliyofanyika mapema alfajiri yaliyosikika mjini sanaa nchini Yemen, yanadaiwa kulenga maeneo nane ya wahouthi.
Soma pia: Marekani na Uingereza zafanya duru mpya ya mashambulizi dhidi ya waasi wa Kihuothi
Uingereza na Marekani waliwashambulia kwa mara ya kwanza waasi hao mapema mwezi huu na Marekani ikaanzisha shambulizi jengine la angani dhidi ya makombora ya wahouthi iliyosema inatoa kitisho kwa raia na meli za kijeshi.
Hata hivyo, waasi hao wameapa kuendelea kushambulia ikiwa ni sehemu moja ya mzozo unaokuwa Mashariki ya Kati unaofungamanishwa na vita vya Israel na Hamas uliozua wasiwasi wa kutanuka kwa vita vitakavyoihusisha Iran.