1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Uturuki

11 Oktoba 2007

Uhusiano kati yxa marekani na Uturuki umekumbwa na msukosuko baada ya Halmashauri ya Baraza la waakilishi la Marekani kupitisha azimio linaloilaani Uturuki kwa mauaji ya waarmenia wakati wa vita vya kwanza vya dunia.

Maandamano juu ya kisa cha waturuki na waarmenia.
Maandamano juu ya kisa cha waturuki na waarmenia.Picha: AP

Mvutano wa kibalozi unapam,bamoto baina ya uturuki na Marekani.Rais mpya wa Uturuki Abdullah Gül, ameieleza kura iliopigwa na Halmasauri ya bunge la Marekani kulaani kile kinachoitwa “kuhilikishwa kwa waarmenia” zaidi ya miaka 90 iliopita wakati wa vita vya kwanza vya dunia ni jambo lisilokubalika.

Uamuzi wa halmashauri hiyo kuwa kuuwawa kwa waarmenia wakati wa enzi za utawala wa Osman ni

“kuhilikisha umma” hakuangaliwi hivyo na waturuki-alisema leo rais Abdullah Gül.

Mbali na kisa cha waarmenia hata vita vya kupambana na ugaidi kinachafua uhusiano kati ya Marekani na mshirika wake wa chanda na pete Uturuki.

Marekani wakati huu inakabiliwa na matatizo mengi na moja kati ya hayo sasa ni uturuki pamoja na vita vya kupambana na ugaidi.Serikali ya Ankara inataka kuwaandama waasi wa kikurdi huko huko kaskazini mwa Irak.Marekani lakini inataka kwa kila hali kuzuwia kujiingiza huko kwa majeshi ya Uturuki.

Seneta Sean McCormack,msemaji wa wizara ya nje ya Marekani asema inahofiwa hapo hatua kama hiyo itaongoza kulivuruga eneo hilo ambalo tangu hapo ni tete.

“Kujiingiza kijeshi kwa Uturuki nchini Irak hakutaongoza kupatikana suluhisho la kudumu.”

Uturuki nayo kwa upande wake inaituhumu Marekani,kuwa haifanyi ya kutosha kupambana na chama cha waasi wa kikurdi cha PKK kinachoendesha harakati zake kaskazini mwa Irak.Hali ya mambo ni mbaya na hakuna kitakachobadilika mnamo muda mfupi ujao.

Halmashauri ya mambo ya nje ya Baraza la waakilishi la Marekani lilipiga kura jana na kuidhinisha kwa sauti 27 dhidi ya 21 azimio ambalo lifikishwe mbele ya Baraza hilo kupiogiwa kura kati ya mwezi ujao.

Azimio sawa na hilo limepelekwa mbele ya baraza la senate.Linalaani kutimuliwa na kuuwawa kwa waarmenia milioni kadhaa.Uturuki ilijaribu kabla kupitishwa azimio hilo kupinga vikali lakini ilikua bure.

Isitoshe,Rais George Bush binafsi aliingilia kati muda mfupi kabla ya kura ya jana katika halmashauri hiyo lakini hakuweza kuzuwia.Alisema:

“Sote tunasikitika kwa msiba uliowafika waarmenia.Lakini kupitisha azimio kama hilo sio njia barabara kama jibu la mauaji hayo.Azimio hilo litachafua usuhuba wetu na mshirika muhimu sana wa NATO na hata kutaleta pingamizi katika vita dhidi ya ugaidi.”

Muda mfupi baadae, waziri wa nje wa Marekani dr.C.Rice alitaja kinaga ubaga hali hasa ilivyo:

Alisema kuwa Marekani inaiihitaji Uturuki kwa sababu ambazo miongoni mwazo kama kambi ya kusafirishia shehena kwa wanajeshi wa Marekani nchini Irak.

Kwa kupitisha azimio hilo, alionya Dr.Rice ,kutatanisha yote ambayo tunayafanya Mashariki ya Kati.

Akaongeza dr.Rice kusema na ninamnukulu,

“Kimkakati tunaiihitaji Uturuki.”

Nafasi ya kuusikiliza mwito huo na kulizima azimio juu ya waarmenia katika Baraza la waakilishi ni ndogo mno.Kwsani,zaidi ya nusu ya wabunge wako nyuma ya azimio hilo.

Katika mjadala uliofanyika katika Halmashauri ya Baraza hilo la waakilishi, ilidhihirika wazi ingawa si ya kufurahisha alao kwa sikio la mjerumani:

Alisema,

Chukulia nchini Ujerumani unaingia madarakani utawala mpya ambao hautambui historia ilivyokwenda na unadai tubomoe makumbusho ya Holocaust.Nani atatuambia kubalini kwavile, tunaihitaji kambi yetu ya wanahewa ya Ramstein.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW