1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Marekani, washirika wapendekeza mpango kusitisha vita Sudan

13 Septemba 2025

Mataifa ya Marekani, Saudi Arabia, Umoja wa falme wa nchi za Kiarabu na Misri yameupendekeza mpango wa miezi wa mitatu wa kufikiwa mapatano ya kusitisha mapigano nchini Sudan.

Mzozo wa Sudan
Vita nchini Sudan vimesababisha maelfu ya raia kuyakimbia makazi yao ndani na nje ya nchi Picha: LUIS TATO/AFP/Getty Images

Nchi hizo zimependekeza pia lengo la usitishaji vita wa kudumu utakaofuatiwa na uongozi wa mpito kwa miezi tisa kuelekea utawala wa kiraia. Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, nchi hizo nne chini ya mwamvuli wao unaojulikana kama Quad, zimesema kipindi cha mpito kinapaswa kukidhi matarajio ya watu wa Sudan kuelekea kuanzishwa kwa urahisi serikali huru, itakayoongozwa kiraia na yenye uhalali mpana na uwajibikaji.

Sudan imekuwa katika vita vya umwagaji damu vya kugombea madaraka tangu mwezi Aprili mwaka 2023 kati ya kiongozi wa kijeshi Abdel-Fattah al-Burhan na makamu wake wa zamani Abdel-Fattah al-Burhananayeongoza vikosi vya RSF.Umoja wa Mataifa umesema machafuko hayo yamesababisha mgogoro mbaya wa kibinadamu ukosefu mkubwa wa chakula wakati maelfu ya watu wamekufa na wengine mamilioni wamelazimika kuyahama makazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW