Marekani: Netanyahu apaswa kuwadhibiti walowezi
30 Oktoba 2023Marekani imemtaka pia Netanyahu kuwawajibisha kwa mashambulizi wanayoyafanya dhidi ya Wapalestina. Awali, Rais wa Marekani Joe Biden, amewatuhumu walowezi hao wa kiyahudi kwa alichokiita ''kumwaga mafuta kwenye moto'' kwa ghasia zinazofanyika katika Ukingo wa Magharibi, wakati Israel ikilipiga vita kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza.
Soma pia: Guterres aonya Gaza inaendelea kuteseka 'kila baada ya saa'
Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak na Rais Emannuel Macron wa Ufaransa wamezungumza jana, na kuahidi kuwa nchi zao zitashirikiana katika kuhakikisha kuwa msaada wa chakula, maji, madawa na mafuta unawafikia wanaouhitaji katika Ukanda wa Gaza.
Kwa mujibu wa wizara ya Afya huko Gaza inayodhibitiwa na Hamas, zaidi ya Wapalestina 8,000 wameuawa tangu kuanza kwa vita hivyo Oktoba 7 mwaka huu.