Usitishwaji mapigano Sudan unaheshimiwa kwa kiwango fulani
26 Mei 2023Matangazo
Hata hiyo, mapigano ya hapa na pale kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF yameripotiwa saa chache zilizopita, na kuathiri utulivu uliokuwepo katika mji mkuu Khartoum.
Mashuhuda aidha wamesema mapigano yametokea leo katika jimbo la Magharibi la Darfur, ikiwa ni siku ya nne ya muafaka wa siku saba wa kuwekwa chini silaha uliosimamiwa na Marekani na Saudia.
Marekani yaonya juu ya ukiukwaji wa makubaliano Sudan
Kwa mujibu wa taasisi ya Armed Conflict and Event Data Project, mapigano hayo yamewauwa watu 1,800 tangu yalipozuka Aprili 15.
Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya Wasudan milioni moja wameyakimbia makazi yao na wengine 300,000 wamekimbilia nchi jirani.