1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAustralia

Australia na Canada kusitisha ufadhili kwa UNRWA

27 Januari 2024

Australia na Canada zimesitisha ufadhili kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Palestina, UNRWA kwa madai kwamba baadhi ya watumishi wake walihusika na shambulizi la Hamas la Oktoba 7.

Ukanda wa Gaza Deir Al Balah | Usambazaji wa chakula na UNRWA
Wapalestina wakiwa wamepanga mistari kusubiri mgao wa unga kutoka kwa shirika la wakimbizi wa Palestina, UNRWA katikati ya vita kati ya Israel na HamasPicha: Ashraf Amra/Anadolu/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong ameandika kwenye ukurasa wa X hii leo kwamba amefedheshwa mno na madai hayo dhidi ya UNRWA na kusema wanazungumza na washirika wao na kusitisha kwa muda ufadhili.

Lakini amezikaribisha hatua za haraka zilizochukuliwa na UNRWA, ikiwa ni pamoja na kusitisha mikataba na kuchunguza madai hayo.

Hatua hiyo inachukuliwa baada ya Marekani kusitisha ufadhili kwa UNRWA siku ya Ijumaa, ikisema madai hayo yalihusisha watumishi 12 ambao "huenda walioshiriki shambulizi hilo" lililochochea vita kati ya Israel na Hamas.