Marekani, Uingereza zataka uchaguzi huru Sudan Kusini
20 Machi 2024Hayo ni katika taarifa ya pamoja kufuatia onyo la Marekani kwamba taifa hilo la Afrika Mashariki haliko katika mwelekeo wa kufanya uchaguzi huru na wa haki, ispokuwa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti.
Mataifa hayo yamesema kuwa kutochukuliwa hatua madhubuti na kutokuruhusu kufanyika kwa uchaguzi huo muhimu ni kushindwa kwa viongozi wa taifa hilo ambalo lilishuhudia mzozo wa kiutawala.
Soma pia:Idadi ya walioathiriwa na ghasia yaongezeka kwa 35% Sudan Kusini
Sudan Kusini inapanga kuchagua viongozi watakaorithi serikali ya mpito ya sasa, inayoongozwa kwa pamoja na Rais Salva Kiir na Makamu wa Kwanza wa Rais Riek Machar, ambao vikosi vyao vilipambana wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mnamo 2013-2018.
Kwa habari nyingine zaidi za ulimwengu, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube.