Marekani: Vikosi vya Iran na Hezbollah vinawasaidia Wahouthi
28 Februari 2024Mjumbe maalum wa Marekani kwa Yemen Tim Lenderking ameiambia kamati ndogo ya baraza la Seneti la Marekani kwamba serikali ya Iran inatoa vifaa na kupiga jeki mashambulizi yanayofanywa na waasi wa Houthi.
Mnamo mwezi Disemba, Ikulu ya White House ilisema kuwa Iran inahusika na kupanga mashambulizi dhidi ya meli za kimataifa katika bahari ya Sham.
Soma pia: Wahouthi washambulia meli nje ya pwani ya Kusini mwa Yemen
Kundi la Wahouthi limeeleza kuwa linafanya mashambulizi hayo kama ishara ya kuonyesha mshikamano na Wapalestina.
Mashambulizi hayo ya Wahouthi yamekuwa na athari kubwa kwa biashara ya kimataifa na kulazimisha baadhi ya kampuni za meli kubadilisha njia na kuzunguka kusini mwa Afrika ili kuiepuka bahari ya Sham.
Wiki iliyopita, Misri ilisema mapato katika mfereji wa Suez yalipungua kwa hadi asilimia 50 mwaka huu.