1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaachana na wazo la jeshi la UM Haiti

30 Septemba 2024

Marekani imeachana na mpango wa kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa libadilishe kikosi cha kimataifa kinachopambana na magenge yenye silaha nchini Haiti kuwa jeshi rasmi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani

Haiti Port-au-Prince | Polisi kutoka Kenya
Maafisa wa polisi wa Kenya wakiwa kwenye operesheni ya usalama nchini Haiti.Picha: Marckinson Pierre/dpa/AP/picture alliance

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaratajiwa kupiga kura juu ya mswada wa azimio ili kuurefusha muda wa kikosi cha hicho kinacholinda amani nchini Haiti hadi tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka ujao.

Jukumu hilo la kulinda amani nchini Haiti lilipitishwa na Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza mwaka uliopita, baada ya nchi hiyo kuomba msaada.

Soma zaidi: Watu 3,661 wameuawa 2024 katika ghasia za Haiti

Kikosi hicho cha kimataifa kinachoongozwa na Kenya kwenye nchi hiyo ya Karibik, hakizingatiwi kuwa operesheni ya Umoja wa Mataifa ingawa kiliidhinishwa na taasisi hiyo.

Urusi na China zinapinga kikosi hicho kuwa jeshi rasmi la Umoja wa Mataifa.   
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW