1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yaadhimisha miaka 250 ya Uhuru wake

4 Julai 2026

Rais wa Marekani Donald Trump katika hotuba yake ya usiku wa kuamkia leo Jumamosi siku ambayo Marekani, inaadhimisha miaka 250, amewaonya raia wake dhidi ya itikadi ya kikomunisti .

Marekani Washington D.C. 2026 | Donald Trump katika hafla ya muungano wa imani na uhuru  huko Washington mnamo Juni 26.
Rais wa Marekani, Donald TrumpPicha: Evan Vucci/REUTERS

Akizungumza mbele ya wafuasi wake kwenye eneo la Kumbukumbu ya Kitaifa ya Mlima Rushmore eneo takatifu lililotengwa kwa ajili ya kuwakilisha msingi, maendeleo na Demokrasia ya Marekani katika jimbo la South Dakota,Trump amesema mtu anaweza kuchagua kati ya kuwa mkomunisti ama mzalendo.

Katika siku za hivi karibuni,  Trump amekuwa akilitumia neno "ukomunisti" kuwakosoa wapinzani wake wa kisiasa wa mrengo wa kushoto na sera zao.

Trump pia ameielezea Marekani kama taifa linalomtegemea Mungu, akisema haki zao wamepewa na Mungu aliyewaumba, na hazitakiwi kuvunjwa.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 80 pia amesema hakuna nchi nyingine iliyoitendea mema zaidi dunia kuliko Marekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW