1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yaahidi dola bilioni 55 kwa Afrika

13 Desemba 2022

Marekani imeahidi dola bilioni 55 kuwekeza kwenye sekta za uchumi, afya na usalama, kusaidia bara la Afrika katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

USA | Präsident Joe Biden
Picha: Nathan Posner/AA/picture alliance

Hayo yamesemwa na Ikulu ya rais nchini Marekani White House, kuelekea mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika.

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuwa mwenyeji wa marais 50 kutoka Afrika mjini Washington leo, mnamo wakati Marekani ikijaribu kuimarisha ushawishi wake barani humo.

Mshauri wa Biden kuhusu usalama wa taifa Jake Sullivan, amesema Marekani inalenga kusaidia nchi za Afrika kufikia malengo yao yenyewe.

Hata hivyo Sullivan hakutoa maelezo zaidi, akisema mengi yatasemwa kwenye mkutano huo wa kilele utakaodumu kwa siku tatu.