Asili na mazingiraAzerbaijan
Marekani yaahidi kuendeleza juhudi, kuzuia ongezeko la joto
12 Novemba 2024Matangazo
Mjumbe wa ngazi za juu wa masuala ya mazingira wa nchini Marekani ameyahakikishia mataifa yanashiriki mkutano wa kimataifa wa mazingira wa COP29 kwamba kurejea kwa rais mteule Donald Trump hakutahitimisha juhudi za taifa hilo za kudhibiti ongezeko la joto duniani.
Mjumbe wa Marekani John Podesta amekiri kwamba utawala ujao wa Marekani utajaribu kubadilisha mkondo, lakini amesema Wamarekani wenyewe watajua namna ya kuikabili hali hiyo.
Licha ya vita nikuvute ya jana Jumatatu baada ya mazungumzo hayo kufunguliwa mjini Baku, serikali ziliidhinisha viwango vipya vya Umoja wa Mataifa vya uzalishaji wa gesi ya kaboni.
Rais wa COP29 Mukhtar Babayev amesifu hatua hiyo iliyofikiwa baada ya miaka kadhaa ya majadiliano magumu.