1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaahidi kusimama na washirika wa NATO

23 Septemba 2025

Marekani imethibitisha kuwa italinda eneo la Jumuia ya Kujihami ya NATO dhidi ya ukiukaji wa mara kwa mara unaofanywa na Urusi wa usalama wa anga wa nchi wanachama wa NATO barani Ulaya.

Bahari ya Baltic 2025 | Ndege za kivita ya Urusi MiG-31
Urusi yatakiwa kuwacha mara moja tabia yake hiyo hatariPicha: Forsvarsmakten/AFP

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Mike Waltz ameuambia mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la umoja huo mjini New York kwamba Marekani inasimama na washirika wake wa NATO katika kukabiliana na ukiukaji huo wa anga.

Waltz amesena Urusi inapaswa kuwacha mara moja tabia yake hiyo hatari, kwani inasababisha kitisho kwa usalama wa Ulaya.

Siku ya Ijumaa, Estonia iliripoti kwamba ndege tatu za kivita za Urusi ziliingia katika anga yake kwa dakika 12.

Hata hivyo, Urusi imekanusha kuhusika na ukiukaji huo.

Aidha, droni kadhaa za Urusi ziliingia katika anga ya Poland wiki moja kabla, wakati wa shambulizi la anga la Urusi nchini Ukraine.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW