Marekani yaahidi msaada wa dola bilioni mbili kwa UN
29 Desemba 2025
Ahadi hiyo ya msaada ni sehemu ndogo ikilinganishwa na kiwango ambacho Marekani imekuwa ikichangia katika miaka ya nyuma. Hata hivyo, serikali ya Marekani inaamini kuwa ahadi hiyo inaashiria kwamba ni mchango mkubwa ulio na uwezo wa kuihifadhi hadhi yake kama mchangiaji mkubwa wa misaada ya kibinadamu ulimwenguni.
Ahadi hiyo ya kufadhili miradi ya msaada wa kiutu inatolewa wakati ambapo makubaliano yaliyo kwenye hatua za mwanzo za mkataba na shirika la Umoja wa Mataifa la Uratibu wa misaada ya kiutu, UNOCHA, linaloongozwa na Tom Fletcher ambaye ni mwanadiplomasia wa zamani wa Uingereza na afisa wa serikali.
Kwa upande wake, mkuu huyo wa UNOCHA, Tom Fletcher, ameyasifu makubaliano hayo na kwenye taarifa yake amefafanua kuwa, "katika kipindi hiki cha majaribu na changamoto kote duniani, Marekani imedhihirisha kuwa ni jabali la kiutu, linalowatia moyo na kuwapa tumaini waliopoteza kila kitu.''
Kimsingi msaada huo unaunda hazina ya pamoja ambayo itayagawia mashirika mbalimbali na miradi hela za ufadhili. Hiki ni kipengee muhimu cha vigezo vya mabadiliko kwenye utaratibu wa Umoja wa Mataifa ambayo yamewashtua wahudumu wengi na kupelekea nafasi za ajira kupotea, miradi na huduma kusitishwa.
Kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa, dola bilioni 2 zilizotangwa ni sehemu ndogo sana ya mchango wa Marekani kwa ufadhili wa miradi ya Umoja wa Mataifa ambayo katika miaka ya hivi karibuni imetumia dola bilioni 17.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, Marekani bado inachangia mabilioni kila mwaka kwa ajili ya uanachama wake katika Umoja wa Mataifa.
Wakati huohuo, Marekani inabainisha kuwa dola bilioni mbili hizo , ni awamu ya kwanza ya kufadhili ombi la hela la kila mwaka la OCHA.
Wafadhili wengine wapunguza misaada
Ifahamike kuwa tayari dhirika hilo lilipunguza kiasi cha fefha inachoomba kwa mwaka huu. Marekani kwa upande wake inasisitiza kuwa Umoja wa Mataifa unalazimika kuziunga pamoja operesheni zake za kiutu ili kupunguza urasimu, miradi kujirudia, na mchepuko wa kiitikadi. Mashirika binafsi yatalahitajika kuendana na hali halisi, kupunguza gharama zao au kufungwa.
Ifahamike kuwa wafadhili wengine wa kigeni kama Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Japan kadhalika wamepunguza viwango inavyotengea misaada na kudai mageuzi kwenye sekta hiyo.
Kwa mtazamo wa wakosoaji, hatua ya mataifa ya kigeni kupunguza misaada haijatathmini athari za baadaye, imewasukuma mamilioni kwenye njaa , mahonjwa au kuyakimbia makaazi yao, na pia kuiondolea Marekani hadhi yake ya kuwa mfadhili mkuu duniani na yenye nguvu ya kivutio.
Yote hayo yakiendelea, mahitaji ya kibinadamu yameongezeka kore ulimwenguni. Ukame umeripotiwa katika baadhi ya maeneo ya Sudan na Gaza yaliyogeuka kuwa uwanja wa vita, mafuriko, njaa na majanga yanayosadikika kuchagizwa na mabadiliko ya tabianchi ambayo yamewasukuma wengi kuyakimbia makaazi yao au kupoteza maisha.
Nchi kadhaa kupokea misaada ikiwemo Kongo
Punguzo hilo la ufadhili litayaathiri mashirika ya Umoja wa Mataifa mfano la Uhamiaji- IOM, Mpango wa Chakula-FAO na la wakimbizi- UNHCR. Tayari yameshabana bajeti zake kwa mwaka huu wa fedha na kupokea kiwango kilichopungya tangu Marekani kubadili uongozi wake.
Kupitia mfumo huu mpya, jumla ya mataifa 17 yatapokea usaidizi kwenye awamu ya kwanza yakiwemo Bangladesh, Kongo, Haiti, Syria na Ukraine.
Afghanistan iliyo hali mbaya haipo kwenye orodha hiyo kama ilivyo Palestina inayoaminika kuwa ifapata usaidizi wa ufadhili wa mradi wa amani wa Gaza unaosimamiwa na Trump. Kimsingi Marekani inataka maslahi yake kupewa kipaumbele hata inapotoa misaada ya kiutu.