Marekani yaahidi msaada zaidi kwa Ukraine
14 Mei 2024Akifafanua zaidi waziri huyo alisema "Tunafahamu hiki ni kipindi kigumu lakini pia tunajuwa hivi karibuni msaada uko njiani. Sehemu ya msaada umeshawasili. Na mwingine zaidi utawasili na utaleta tofauti kubwa katika kukabiliana na uchokozi unaoendelea wa Urusi katika uwanja wa mapambano. Na tumejidhatiti pamoja na washirika wengine wengi wa Ukraine kuhakikisha kwamba mnafanikiwa katika uwanja wa mapambano. Halikadhalika tumedhatiti kwa muda kuona Ukraine inasimama imara kivyake.'' Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za Juu wa Marekani aliyeko katika ziara ambayo haikutangazwa mjini Kiev amefanyamazungumzo na rais Volodymyr Zelensky ambaye ameomba nchi yake ipatiwe mifumo zaidi ya ulinzi kuwalinda raia dhidi ya mashambulizi ya Urusi Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo. Urusi imekamata eneo la ukubwa wa takriban kilomita 125 za mraba ambalo linajumuisha vijiji vipatavyo saba kwa mujibu wa taarifa ya vyanzo vinavyofuatilia matukio katika eneo hilo.Ziara ya Blinken imelenga kumpa uhakika mshirika wake Ukraine katika vita hivyo vya Urusi.