1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Israel na Lebanon wameafikiana kusitisha vita

25 Novemba 2024

Israel na Lebanon zimekubaliana juu ya mapendekezo ya kusimamisha mapigano na kuumaliza mzozo kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hezbollah.

Mzozo nchini Lebanon
Makabiliano kati ya Israel na wanamgambo wa kundi la Hezbollah la Lebanon yamesababisha maafa makubwa. Picha: AFP

Hayo yameelezwa na shirika la habari la Axios lililomnukuu afisa mwandamizi wa Marekani ambaye jina lake halikutajwa.

Serikali ya Israel imesema leo inaelekea kufikia makubaliano ya kusitisha vita na Hezbollah japo kulikuwepo na masuala ambayo bado yanapaswa kushughulikiwa.

Maafisa wa Lebanon licha ya tamko la Israel, wameonyesha matumaini ya tahadhari wakisema Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu sio mtu wa kuaminiwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW