1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

US yachunguza kuvuja nyaraka za shambulio la dhidi ya Iran

Angela Mdungu
20 Oktoba 2024

Spika wa baraza la wawakilishi la Marekani Mike Johnson amebainisha kuwa uchunguzi kuhusu nyaraka za siri zilizovuja zinazohusu maandalizi ya mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran unaendelea.

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Mike Johnson
Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Mike JohnsonPicha: Ebrahim Noroozi/AP/picture alliance

Akizungumza na shirika la habari la CNN la Johnson ameeleza kuwa wanalifuatilia kwa karibu suala hilo bila ya kutoa taarifa zaidi. Kulingana na afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutajwa jina, nyaraka zilizovuja zinaonekana kuwa halali.

Soma zaidi: Israel yasema 'maslahi ya taifa' kwanza katika kuijibu Iran

Nyaraka hizo zilizokuwa na mhuri unaoonesha kuwa ni za siri, zilichapishwa kwenye jukwaa la Telegram na kisha ziliripotiwa pia na vituo vya Habari vya CNN na Axios.

Soma zaidi:Iran yaahidi kuishambulia miundo mbinu ya Israel iwapo itashambuliwa 

Upelelezi una unaofanywa kuhusu kuvuja kwa taarifa hizo unachunguza pia namna nyaraka hizo zilivyopatikana aidha kwa makusudi, au kwa njia nyingine kama vile udukuzi. Kama sehemu ya uchunguzi huo, maafisa wanachunguza pia kufahamu mtu aliyehusika kuzipata nyaraka hizo kabla ya kuchapishwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW