1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yadungua kifaa kingine katika anga yake

13 Februari 2023

Marekani imedungua kifaa kingine ambacho hakijatambuliwa katika anga yake eneo la Ziwa Huron, kufuatia amri ya rais wa nchi hiyo Joe Biden.

Südchinesisches Meer | US Kampfjet
Picha: Mcs Leon Vonguyen/Planetpix/ZUMA Wire/IMAGO

Ikulu ya Marekani White House, imesema vitu hivyo vinavyoruka vilikuwa vidogo zaidi kuliko   puto la Chinalililodunguliwa wiki iliyopita. China hata hivyo ilisisitiza kuwa puto hilo lilikuwa purutangi au puto kubwa la kiraia linalotumika kwa ajili ya utafiti.

Mkuu wa kamandi ya Marekani iliyoko kaskazini mwa nchi hiyo Jenerali Glen VanHerck, amewaambia waandishi wa habari kwamba sehemu ya sababu ya kudungua vifaa hivyo, ni kuimarishwa kwa hali ya tahadhari baada ya puto la kijasusi la  China  kugunduliwa kwenye anga ya Marekani mwishoni mwa mwezi Januari.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW