Marekani yafanya mashambulizi mapya nchini Iran
13 Julai 2026
Katika chapisho kwenye mtandao wa X, kamandi Kuu ya Jeshi hilo la Marekani CENTCOM, imesema mashambulizi hayo mapya yalianza saa tisa usiku kwa majira ya eneo hilo, baada ya kutangaza awali kuwa ilikuwa imefanya takriban mashambulizi 140 usiku uliotangulia.
kwa upande wake, Iran imeripoti kuwa visiwa vyake viwili vya kusini pia vimeshambuliwa, huku Kuwait ambako mara kwa mara Iran imekuwa ikilenga vituo vya kijeshi vya Marekani, ikisema vituo vya ulinzi mpakani na kituo cha mafuta cha baharini vilishambuliwa.
Mapigano hayo mapya yalifuatia shambulio la Iran mapema Jumapili dhidi ya meli ya kibiashara katikaujia huo wa bahari, ambapo wafanyakazi wake walilazimika kuitelekeza baada ya kushika moto.
Baada ya tukio hilo, Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu cha Iran (IRGC) kilitangaza kuwa Mlango-Bahari wa Hormuz utafungwa hadi itakapotolewa taarifa nyingine.