1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yashambulia ngome kuu za kundi la IS, Syria

11 Januari 2026

Marekani imeanzisha mashambulizi mengine ya kulipiza kisasi dhidi ya kundi linalojiita Dola la Kiislamu Syria, kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi hilo lililosababisha mauaji ya wanajeshi wa Marekani.

USA 2025 | US-Soldat befestigt GBU-31-Bombe an einem F-15E Strike Eagle Kampfjet
Marekani yafanya mashambulizi ya kulipiza kisadi dhidi ya IS, SyriaPicha: U.S. Air Force/REUTERS

Shambulizi hilo lililofanywa kwa usaidizi wa washirika wa kijeshi wa Marekani limezilenga ngome za IS kote nchini Syria. Jeshi la Jordan lilitangaza kushiriki katika mashambulizi hayo.

Mashambulizi hayo ya jana Jumamosi ni sehemu ya hatua ya kujibu mapigo iliyochukuliwa na  rais wa Marekani Donald Trump dhidi ya shambulizi la ISIS lililomuua sajenti Edgar Brian Torres-Tovar, sajenti William Nathaniel Howard, na Ayad Mansoor Sakat, katika eneo la Palmyra.

Marekani imeendelea kusema kwamba inatoa ujumbe mzito kwa yeyote atakayewadhuru wapiganaji wa Marekani kwamba watatafutwa na kuuawa kokote pale walipo.

Siku moja kabla ya shambulizi hilo afisa mmoja wa Syria alisema vikosi vya taifa hilo vimemkamata kiongozi wa operesheni za IS.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW