Marekani yafungua ubalozi wake Somalia
3 Oktoba 2019Marekeni imesema kuwa imeufungua ubalozi wake nchini Somalia takriban miongo mitatu baada ya nchi hiyo kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe na jeshi la Marekani kumchukuwa balozi wake kwa ndege na kumhamishia katika eneo salama.
Taarifa iliyotolewa hapo jana jioni inasema kuwa hatua ya kufunguliwa kwa ubalozi huo inaonyesha ufanisi wa hivi punde katika taifa hilo la Pembe ya Afrika ambalo bado linakabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa wanamgambo wa al-Shabab walio na ushirikiano na kundi la al-Qaida.
Siku ya Jumatatu, kundi la al-Shabab lilijaribu kuuvamia uwanja wa ndege za kijeshi wa Belidogle Kusini mwa Somalia ulio na vikosi vya kijeshi vya Somalia na Marekani na unaotumika kuzirusha ndege zisizokuwa na rubani zinazolishambulia kundi hilo.
Ubalozi huo ulifunga shughuli zake mjini Mogadishu mwaka 1991.