Marekani yahimiza haki za wafanyakazi wa bandarini
2 Oktoba 2024Wito huo umetolewa wakati wafanyakazi wa bandarini katika pwani ya mashariki na pwani ya ghuba ya Marekani wakianza mgomo wao wa kwanza mkubwa kabisa katika kipindi cha miaka 50.
Msemaji wa ikulu ya Marekani, Karine Jean-Pierre, amesema kampuni za meli zimefanikiwa kuweka rekodi kwa kupata faida tangu janga la korona na baadhi zimeshuhudia faida zao zikikua kupita kiwango cha asilimia 800 ikilinganishwa na faida zao kabla janga hilo.
Soma zaidi: Watu 600 hawajulikani walipo North Carolina
Malipo ya marupurupu kwa wakuu wa makampuni hayo imeongezekana kutokana na faida hizo na wamiliki wa hisa nao pia wamenufaika sana.
Jean-Pierre amesema ni haki kwa wafanyakazi wanaohatarisha maisha yao kuhakikisha bandari zinaendelea kufanya kazi wapate nyongeza ya maana katika mishahara yao.