1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaidhinisha chanjo ya Chikungunya

10 Novemba 2023

Maafisa wa afya nchini Marekani wameidhinisha kwa mara ya kwanza ulimwenguni chanjo dhidi ya homa ya Chikungunya.

Mbu anaesababisha magonjwa kwa binaadamu kama Malaria na Chikungunya
Mbu anaesababisha magonjwa kwa binaadamu kama Malaria na Chikungunya Picha: Robin Loznak/ZUMA/picture alliance

Kulingana na mamlaka inayosimamia chakula na dawa (FDA) ya marekani, chanjo hiyo ambayo imepewa jina la Ixchiq iliyotengenezwa na kampuni ya Ulaya, Valneva, imeidhinishwa kutolewa kwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi walioko katika hatari kubwa ya kuambukizwa.

Tanzania yakiri kuwa na Chikungunya, Dengue

Uidhinishwaji wa chanjo hiyo unatarajiwa kuharakisha usambazwaji wa dozi za chanjo hiyo katika nchi ambazo virusi hivyo vimeenea zaidi hasa Afrika, kusini mashariki mwa Asia na nchi za Amerika.

Chikungunya, husababisha homa na maumivu makali ya viungo.

Virusi vyake huenezwa na mbu  na wataalam wa dawa wanavitaja kuwa “tishio la afya linaloongezeka duniani”.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW