1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaidhinisha uuzaji wa vifaa vya kijeshi kwa Taiwan

30 Juni 2023

Marekani imefahamisha jana kuwa inapanga kuiuzia Taiwan zana na vifaa vya kijeshi vyenye thamani ya dola milioni 440 katika sehemu ya juhudi zake za hivi punde za kuimarisha ulinzi wa kisiwa hicho kinachojitawala.

China-Taiwan Militärübung
Picha: picture alliance/Xinhua News Agency

 

Hata hivyo, uuzaji huu ni mdogo kuliko ilivyotarajiwa na hautahusisha aina kadhaa za silaha za Marekani, lakini unajiri wakati Marekani na China zikijaribu kuleta utulivu katika mahusiano yao yenye misukosuko.

China inayodai kuwa kisiwa hicho ni sehemu ya himaya yake, imelaani vikali hatua hiyo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Mao Ning amesema Marekani inapaswa kuachana na harakati zozote zinazoweza kuibua upya mvutano wa kijeshi katika eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW