Marekani yaihakikishia Qatar usalama wake
1 Oktoba 2025
Matangazo
Ikulu ya Marekani, White House imesema kuwa pia itaihakikishia Qatar usalama wake.
Amri ya Kiutendaji iliyosainiwa Jumatatu na Rais Donald Trump, imetolewa Jumatano, baada ya Israel kuishambulia Qatar, mshirika muhimu wa Marekani mwezi uliopita.
Ikiwezakana Marekani itachukua hatua za kijeshi
Marekani imesema katika shambulizi lolote dhidi ya Qatar, nchi hiyo itachukua hatua halali na zinazofaa, ikiwemo kidiplomasia, kiuchumi na ikilazimika kijeshi ili kulinda maslahi ya Marekani na Qatar, na kurejesha amani na utulivu.
Siku ya Jumatatu Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alimpigia simu Waziri Mkuu wa Qatar kutokea White House na kuomba radhi kutokana na mashambulizi hayo na kuahidi kutojirudia tena.
Netanyahu alikuwepo mjini Washington kwa ajili ya kukutana na Trump.