Marekani yaihakikishia Ukraine kupata msaada wa kijeshi
19 Aprili 2024Matangazo
Waziri Mkuu huyo amesema maafisa wa Washington wameihakikishia serikali mjini Kyiv kuwa, wangelipata silaha mpya katika siku za usoni mara baada ya msaada huo kuidhinishwa.
Aidha Shmyhal ameongeza kwamba viongozi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, Benki ya Dunia na maafisa wa fedha kutoka mataifa mbalimbali wamesisitiza juu ya uungwaji mkono kwa Ukraine unasalia kuwa kipaumbele wakati ikiendelea kupambana na uvamizi wa Urusi.
Soma pia:Marekani yaionya China dhidi ya ushindi wa Urusi kwenye vita vya Ukraine
Amewaambia waandishi wa habari kuwa maafisa nchini Ukraine wamekuwa na mazungumzo ya jinsi ya kutumia amana za Urusi zinayoshikiliwa, ili kuinufaisha Ukraine na mwaka huu wanatarajia kupata matokeo juu ya mazungumzo hayo.