1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaihimiza Uingereza kutolitambua taifa la Palestina

20 Septemba 2025

Wanasiasa wa Marekani wameionya Uingereza na washirika wake wengine dhidi ya kuitambua Palestina kama dola huru, wakisema hatua hiyo itawapa nguvu wanamgambo wa Hamas na kutishia usalama wa Israel.

Elise Stefanik
Mbunge wa New York, Elise StefanikPicha: Alex Brandon/AP/picture alliance

Wanasiasa hao wa chama cha Republican akiwemo mbunge wa New York Elise Stefanik na seneta Rick Scott, wameyatumia barua mataifa ya Uingereza, Ufaransa, Canada na Australia pamoja na washirika wengine muhimu,  wakiwataka kupinga juhudi katika mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa za kuihalalisha na kuitambua Palestina kama dola huru.

Stefanik na Scott wamesema kulitambua taifa la Palestina kunaweka kielelezo cha hatari kwamba vurugu na wala sio diplomasia, ndio njia inayofaa kwa makundi ya kigaidi kama Hamas kufikia malengo yao ya kisiasa.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa kutangaza rasmi uamuzi wa nchi yake kuitambua Palestina kesho Jumapili.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW