1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yailaani M23 kwa kuvunja usitishaji mapigano

7 Januari 2025

Marekani imelaani 'uvunjaji wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano' wa kundi la waasi la M23 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambao mwishoni mwa wiki waliutwaa mji muhimu mashariki mwa nchi hiyo.

DR Kongo | M23
Mwanajeshi wa kundi la waasi la M23 akiwa karibu na mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Arlette Bashizi/REUTERS


Taarifa iliyotolewa jana na msemaji wa Wizara ya Mambo ya Kigeni ya Marekani, Mathew Miller, imesema kwamba kusonga mbele wa M23, kukiwemo kuutwaa mji huo wa Masisi, kunaharibu juhudi za kupatikana kwa amani mashariki mwa Kongo na pia kuwadhuru na kuwageuza raia kuwa wakimbizi.

Msemaji huyo alisema M23 wanapaswa kuacha mara moja harakati zao za kiuchokozi na kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano.

Soma zaidi: Waasi wa M23 waudhibiti mji wa kimkakati wa mashariki ya Kongo

Kundi hilo linaloungwa mkono  na Rwanda limechukuwa maeneo makubwa ya mashariki mwa Kongo tangu mwaka 2021, na kusababisha maafa na mzozo mkubwa wa wakimbizi.

Marekani imeitaka tena Rwanda kuondowa wanajeshi wake ndani ya ardhi ya Kongo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW